- Balala asema ubunifu sasa ndio suluhisho la kuimarisha sekta ya utalii siku zijazo
- Sekta ya utalii imepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 80 kwa ajili ya Corona
Ubunifu sasa unafaa kuwa jambo la msingi kwa wadau katika sekta ya utalii ,amesema waziri wa Utalii Najib Balala .
Katika mkutano uliofanywa kwa njia ya kidijitali siku ya jumanne Balala amesema wafanyikazi katika sekta hiyo wanafaa kupewa upya mafunzo ,kuwa wabunifu na kuvumbua mbinu mpya za kufanikisha utalii ili kusalia katika sekta hiyo .
" Huu ndio wakati wa kustahimili na kubadilisha jinsi ya kuendesha oparesheni na utoaji wa huduma katika sekta hii ili kuifanya kuwa thabiti katika siku zijazo’ amesema
Balala amesema sekta hiyo italazimika kutathmini kuhusu masuala muhimu kama vile afya na matumizi ya teknolojia pamoja na kuzihusisha jamii kwa kuzinufaisha moja kwa moja ili kustahimili changamoto zijazo.
Kenya imepewa muhuri wa kimataifa wa baraza l dunia la usafiri na utalii kwa kuanzisha mikakati na hatua za kudumisha usalama wa kiafya katika shughuli zake za kitali .
Sekta ya utalii ni mojawapo ya zilizoathiriwa pakubwa na janga la Corona na Balala amesema mapato ya Utalii yamepungua kwa asilimia 98 na kusajili hasara ya Zaidi ya shilingi bilioni 80