Omtatah asimamakidete

Omtatah awasilisha kesi nyingine kumzuia Mwilu kuchukua usukani kama kaimu jaji mkuu

Amesema Maraga hana maamlaka ama uwezo wa kumetua kaimu jaji mkuu

Muhtasari
  • Omtatah  amesema hatua hiyo ya Maraga kumteua naibu wake kutwaa majukumu yake kama jaji mkuu kuanzia disemba tarehe 12  ni ukiukaji wa sheria na katiba .
  •  Mwanaharakati huyo anataka mahakama kutoa agizo la  muda kuzuia uamuzi wa jaji mkuu kusalimisha mamlaka yake kwa Mwilu hadi ombi lake lisikizwe.
Jaji Mkuu David Maraga akishauriana na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Jaji Smokin Wanjala wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 14, 2017. Picha: JACK OWUOR
Jaji Mkuu David Maraga akishauriana na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Jaji Smokin Wanjala wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 14, 2017. Picha: JACK OWUOR

 Mwanaharakati Okiya Omtatah amewasilisha kesi nyingine kortini  akitaka kumzuia naibu jaji mkuu Philomena Mwilu dhidi ya kuchukua usukani kama kaimu jaji mkuu .

 Mwanaharakati huyo  anapinga uamuzi wa jaji mkuu anayeondoka David Maraga kumkabidhi Mwilu madaraka yake hadi tume ya JSC itakapomteua jaji mkuu mpya .

Omtatah  amesema hatua hiyo ya Maraga kumteua naibu wake kutwaa majukumu yake kama jaji mkuu kuanzia disemba tarehe 12  ni ukiukaji wa sheria na katiba .

Okiya Omtatah
Okiya Omtatah Okiya Omtatah

 Amesema Maraga hana maamlaka ama uwezo wa  kumetua kaimu jaji mkuu  kwa sababu hakuna kipengee katika katiba  kinachompa maamlka ya kumteua kaimu jaji mkuu .

 Bwana Omtatah pia amedai kwamba nafasi ya kaimu jaji mkuu inakiuka katiba kwani ni mtu mmoja tu anayetambuliwa kama jaji mkuu . Hata naibu jaji mkuu hufanya kazi chini ya maelekezo ya jaji mkuu

 Mwanaharakati huyo anataka mahakama kutoa agizo la  muda kuzuia uamuzi wa jaji mkuu kusalimisha mamlaka yake kwa Mwilu hadi ombi lake lisikizwe.