wizi

Mfanyikazi wa nyumbani ashtakiwa kwa wizi wa shilingi laki tatu kileleshwa

Kesi hiyo itatajwa januari tarehe 21.

Muhtasari
  • Luyeku  anashtumiwa kwa kuiba pesa hizo kutoka kwa Joyce Kayere katika  tarehe mbali mbali kati ya oktoba 10 na 27 mwaka hiyo .
  • Aliachiliwa kwa bondi ya shilingi laki tatu au dhamana ya shilingi elfu 150.
Consolata Luyeku

 Mfanyikazi  mmoja  wa nyumbani  ameshtakiwa kwa wizi wa shilingi laki tatu  kutoka kwa mwajiri  wake mtaani  kileleshwa .

Consolata Luyeku  amefikishwa  katika mahakama ya kibera   mbele  ya hakimu mkuu  Derrick Kuto .

Luyeku  anashtumiwa kwa kuiba pesa hizo kutoka kwa Joyce Kayere katika  tarehe mbali mbali kati ya oktoba 10 na 27 mwaka hiyo .

Pia alishtakiwa kwa kosa la pili la kumiliki nguo za kayere zenye thamani ya shilingi elfu 50 .

 Mtuhumiwa  anadaiwa kujaribu  kuwasiliana nan a mlalamishi

Aliachiliwa kwa bondi ya shilingi laki tatu au dhamana ya shilingi elfu 150.

Kesi hiyo itatajwa januari tarehe 21.