Shule

Matakwa ya walimu wakuu kabla ya shule kufunguliwa Januari

Waziri wa elimu George Magoha amekiri kwamba kuwatenganisha wanafunzi ili wasikusanyike katika sehemu moja wakiwa shuleni ndio changamoto kubwa

Muhtasari
  •  Walimu wakuu wanasema ili shule kufunguliw ana kuendelea na oparesheni kikamilifu serikali na wazazi wanafaa kuhakikisha kwamba kuna fedha .
  • Indimuli Kahi,  mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili  amesema bila fedha  shughuli za kurejelea masomo zitalemazwa hasa  katikati ya janga la Corona .

Shule zitachukua likizo  wiki ijayo kwa sherehe za krisimasi kabla ya kufunguliwa kwa muhula mwingine mwezi januri .

 Walimu wakuu wanasema ili shule kufunguliw ana kuendelea na oparesheni kikamilifu serikali na wazazi wanafaa kuhakikisha kwamba kuna fedha .

Indimuli Kahi,  mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili  amesema bila fedha  shughuli za kurejelea masomo zitalemazwa hasa  katikati ya janga la Corona .

 Pia panafaa kuwa na mikakati ya kuwarejesha shuleni wanafunzi ambao huenda wameacha shule baada ya kuwa nje kwa muda huo mrefu tangu shule kufungwa mwezi machi mwaka huu kwa ajili ya Corona .

 Walimu hao wakuu pia wanataka kupewa mafunzo kwa walimu  na wanafunzi kuhusu jinsi ya kukabiliana na virusi vya Corona  .mafunzo hayo Kahi amesema  yanafaa kupigwa jeki na msaada wa kila mara wa ushauri  na usaidizi wa kisaikolojia .

 Kahi amesma pia walimu watakabiliwa na changamoto ya kuzuia mrundiko wa wanafunzi wengi madarasani ili kuzuia wanafunzi kuambukizana virusi hivyo .

 Walmu katika mapendekezo yao wanataka masomo kufanywa nje ya darasa  na masomo ya ziada kwa wanafunzi wa madarasa ya juu kuruhusiwa  .

Waziri wa elimu George Magoha  amekiri kwamba kuwatenganisha wanafunzi ili wasikusanyike katika sehemu moja wakiwa shuleni ndio changamoto kubwa