- Amewataka viongozi kuwaruhusu wakenya kusoma na kuelewa mapendekezo yaliotolewa kuirekebisha katiba bila kuwapa vitisho .
- Amesema viongozi wanafaa kuwaelimisha wakenya kuhusu vipengee vya sheria vilivyorekebishwa badala ya kufanya kampeni za kupinga ama kuunga mkono kura ya maamuzi kuhusu mapendekezo hayo .
Naibu wa rais William Ruto amewahimiza viongozi kutotumia BBI kuwagawanya wakenya .
Amewataka viongozi kuwaruhusu wakenya kusoma na kuelewa mapendekezo yaliotolewa kuirekebisha katiba bila kuwapa vitisho .
Amesema viongozi wanafaa kuwaelimisha wakenya kuhusu vipengee vya sheria vilivyorekebishwa badala ya kufanya kampeni za kupinga ama kuunga mkono kura ya maamuzi kuhusu mapendekezo hayo .
“ Marekebisho ya katiba hayafai kuwagawanya wakenya na kuzua uhasama’ amesema Ruto .
Dr Ruto aliyasema hayo siku ya jumatano wakati wa mazishi ya Nalangu Enole Ntutu, mamake seneta wa zamani wa Narok Stephen Ole Ntutu na mshirikishi wa wizara ya Leba Patrick Ole Ntutu katika boma lao Ololunga ,kaunti ya Narok
Alikuwa ameandamana na waziri wa Leba Simon Chelgui, magavana Samuel Tunai (Narok), Hillary Barchok (Bomet) na Joseph Ole Lenku (Kajiado), wabunge Korei Ole Lemein (Narok South), Soipan Tuya (Narok) na David Ole Sankok (Mteule ).
Wengine walikuwa Johana Ng'eno (Emurua Dikirr) Ndindi Nyoro (Kiharu), Benjamin Washiali (Mumias East).