Mauaji ya krisimasi

Polisi wachunguza mauaji ya afisa wa KDF

Afisa wa KDF alimsalimia mwanamke mmoja

Muhtasari
  • Tayari watu sita wamekamatwa  kuhusiana na tukio hilo na watafikishwa kortini leo .
  •  Aliuawa kwa kupigwa mawe na  kundi moja la watu ambao alikuwa amelumbana nao akitembea kutoka baa moja .

 Polisi wanachunguza tukio la mauaji ya afisa wa KDF mwenye umi wa miaka 38 aliyeshambuliwa na umati wa watu siku ya krisimasi mtaani Utaweala ,Nairobi .

 Aliuawa kwa kupigwa mawe na  kundi moja la watu ambao alikuwa amelumbana nao akitembea kutoka baa moja .

 Polisi wanasema uchunguzi wa mwanzo unaonyesha kwamba afisa huyo na kakake walikuwa wakitoka baa moja walipokutana na  kundi hilo lililowashambulia .

Inadaiwa mwanajeshi huyo alimsalimua mwanamke mmoja hatua ambayo ilimhamakisha mpenzi wa mwanamke huyo  na hapo ndipo ugomvi ulipozuka  na baadaye kusababisha kuuawa kwa mwanajeshi huyo kwa kupigwa mawe  wakati mtu na mpenzi wake walipopigwa ukemi kwamba wanashambuliwa na majambazi .  Tayari watu sita wamekamatwa  kuhusiana na tukio hilo na watafikishwa kortini leo .