Covid-19: Watu 6 waaga dunia kutokana na corona

Muhtasari
  • Watu 141 wapatikana na corona huku 25 wakiwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi ICU
  • Pia watu 6 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo
  • Idadi ya waliopona imefika  83,625 baada ya watu 207 kupona hii leo

Kenya hii leo imesajili visa 141 vipya vya maambukizi ya corona huku maambukizi ya maradhi hayo yakifikia 100,193

Hii ni baada ya sampuli 3,571 kupimwa chini ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya 121 ni wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni.

 

81 ni wanaume huku 60  wakiwa ni wanawake,mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa chini akiwa na miaka 87.

Vile vile watu 207 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 83,625 ya watu waliopona corona.

Watu 192 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 15 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Wagonjwa 500 wamelazwa hospitalini tofauti humu nchini huku 1,340 wakiwa wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri watu 6 amepoteza maisha yake kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 1,750 watu waliada kutokana na corona

Pia wagonjwa 25 wamo katika wadi wa wagonjwa mahututi (ICU).