Matayarisho ya KCPE na KCSE

Zaidi ya maafisa 286,000 kusimamia mitihani ya KCPE na KCSE

Katika mitihani ya mwaka huu knec imetumia kontena 479 katika makao makuu ya kaunti ndogo ili kuhifadhi karatasi za mtihani .

Muhtasari
  •  Watahiniwa   1,191,411 wamesajili kufanya mtihani wa KCPE katika vituo   28,451
  •  Watahiniwa  752,933 wamesajiliwa kufanya KCSE katika vituo   10,437  ikilinganishwa na vituo  10,287 mwaka wa 2019
Waziri wa elimu George Magoha

 Kutakuwa na idadi kubwa ya maafisa watakaotumwa katika vituo vya mitihani ya kitaifa ili kuhakikisha kwamba inafanywa kwa ufanisi hasa kwa ajili ya janga la sasa la Corona

 Baraza la kitaifa la mtihani  KNEC limesema  Zaidi ya maafisa 286,901 wa nyanjani watatumiwa kusimamia mitihani hiyo  ikilinganishwa na  idadi ya maafisa 173,000 waliotumiwa mwaka wa 2019 .

 Maelezo hayo yamo katika  ripoti ya matayarisho ya kufanywa kwa mitihani ya kitaifa .  mitihani ya mwaka huu ya KCPE na KCSE itafanywa mwezi machi na Aprili .kwa kawaida mitihani hiyo hufanywa  kati ya Oktoba na Novemba .

 Watahiniwa   1,191,411 wamesajili kufanya mtihani wa KCPE katika vituo   28,451

 Watahiniwa  752,933 wamesajiliwa kufanya KCSE katika vituo   10,437  ikilinganishwa na vituo  10,287 mwaka wa 2019

 Kufuatia kipindi kirefu ambapo shule zilifungwa KNEC intarayarisha takwimu za shule ambazo zilifungwa na watahiniwa  kuathiriwa . Miongoni mwa changamoto ambazo huenda zikatokea wakati wa mitihani hiyo ni msimu wa mvua . Baraza la mtihani pia linahofia hali mbaya ya usalama  na mafuriko katika maeneo kadhaa huenda zikasababisha usumbufu wakati wa mtihani .

 Katika mitihani ya mwaka huu knec imetumia kontena 479 katika makao makuu ya kaunti ndogo ili kuhifadhi karatasi za mtihani .