- Waziri wa elimu George Magoha wiki jana alipendekeza kurejeshwa kwa dhabu ya viboko shuleni ili kukabiliana na visa vya ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi .
- Waziri huyo pia alilalamikia ongezeko la visa vya wanafunzi kuzichoma shule zao na kuwashambulia walimu .
Muungano wa walimu nchini KNUT umeapa kupinga kurejeshwa kwa adhabu ya kuchapwa viboko shuleni ukisema hatua hiyo italeta malumbano kato ya walimu na wanafunzi .
Katibu mkuu wa KUT Wilson Sossion amesema kurejeshwa kwa adhabu hiyo kutahatarisha maisha ya walimu hasa kutoka kwa wanafunzi ambao sasa ndio wanaingia umri wa kubaleghe
Ameitaka serikali kuziondoa shule za mabweni ili kila mzazi atekeleze jukumu la kumuadhibu mtoto wake .
Sossion wakati huo huo pia ameishtumu serikali kwa kuifanya dhaofu miungano ya wafanyikazi ili kuwatumia vibaya wafanyikazi .Amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili kumaliza malumbano kati ya KNUT na TSC .
Waziri wa elimu George Magoha wiki jana alipendekeza kurejeshwa kwa dhabu ya viboko shuleni ili kukabiliana na visa vya ukosefu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi .
Waziri huyo pia alilalamikia ongezeko la visa vya wanafunzi kuzichoma shule zao na kuwashambulia walimu .
‘Adahabu ya viboko ikitumiwa vizuri inaweza kupunguza kabisa visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa wanafunzi ‘ alisema Magoha .
Aliwashauri wazazi kupambana na wanao wakiwa nyumbani ili kupunguza utundu wao wakiwa shuleni .