- Mwanasiasa huyo aliyehudumu kama mkuu wa mkoa amekuwa hospitali kwa muda wa Zaidi ya mwezi mmoja .
- Rais alisema mbunge huyo wa zamani wan Nyaribari Chache alikuwa mtu mcheshi ,alipatikana kwa urahisi na mzee wa kutegemewa
Familia na marafiki wa waziri wa zamani Simeon Nyache wamemtaja kama kiongozi ambaye alikuwa na maono makubwa na aliyekuwa akifuata kila kanuni za nidhamu . Nyanchae ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88 .
Wake zake wawili Martha na Grace walijawa na huzuni wakati walipofika katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee . Mwanawe ,mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya kiutekeleza katiba Charles Nyachae na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I waliongoza familia katika kutangaza kifo cha Simeon Nyachae .
" Sote tumempoteza baba na kielelezo’ Matiang’I alisema baada ya Charles kutoa Habari za kifo cha babake .
Mwanasiasa huyo aliyehudumu kama mkuu wa mkoa amekuwa hospitali kwa muda wa Zaidi ya mwezi mmoja . Familia yake imesema aliaga dunia kutokana na ugonjwa ambao amepambana na ‘kwa ujasiri’
Rais Uhuru Kenyatta amemtaja Nyachae kama kielelezo cha maendeleo nchini kupitia miaka yake mingi katika utumishi wa umma . Kupitia taarifa Uhuru alijutia kifo cha Nyachae akisema kwamba alikuwa kiongozi wa taifa mwenye busara ambaye utumishi kwa nchi uliaidia kuifanya Kenya kuwa kitovu cha ustawi katika bara la Afrika .
Rais alisema mbunge huyo wa zamani wan Nyaribari Chache alikuwa mtu mcheshi ,alipatikana kwa urahisi na mzee wa kutegemewa
Katibu wa usimamizi wa wizara ya Uchukuzi na miundo msingi alikitaja kifo cha Nyache kama hatua ambayo imeacha jamii ya Gusii katika hali mbaya .
Rais wa zamani Mwai Kibaki amemtaja Nyache kama mmoja wa watumishi wenye bidii wa umma Kenya . Nyachae aliwahi kuhudumu kama waziri Fedha ,Kawi na baadaye Barabara na ujenzi wa umma .