Covid-19: 129 wapatikana na corona,59 wapona huku 3 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Watu 129 wapatikana na virusi vya covid-19, huku 37 wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi( ICU)
  • Huku hayo yakijiri watu 3 wamepoteza maisha ya kutokana na corona huku idadi ya waliofariki ikifika 1,779
  • Pia watu 59 wamepona corona idadi jumla ya waliopona sasa imefika 84,361

Kufikia Jumapili ya leo idadi ya maambukizi ya corona mefika 101,819 baada ya watu 129 zaidi kuparikana na corona.

Hii ni baada ya sampuli 4,797 kupimwa ndani ya saa 24, kati ya maambukizi hayo mapya 96 ni wakenya ilhali 33 ni raia wa kigeni.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 81, 69 ni wanaume ilhali 60 ni wanwake.

Huku hayo yakijiri watu 3 wamepoteza maisha ya kutokana na corona huku idadi ya waliofariki ikifika 1,779

Pia watu 59 wamepona corona idadi jumla ya waliopona sasa imefika 84,361,25 wameruhuriwa kuenda nyumbani kutoka hospitali mbalimbali nchini ilhali wengine 34 wamepina wakiwa wamejitenga nyumbani.

Wagonjwa 391 wamelazwa hospitalini ilhali 1,378 wamejitenga nyumbani.

Wagonjwa 37 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi(ICU).