Mauaji Laikipia

Polisi Laikipia wachunguza mauaji ya mwanamke

Mwili wake ulipatikana katika chumba chake cha kulala na inashukiwa aliuawa na watu waliomkata shingoni na kutoroka .

Muhtasari
  • Mwili wake ulipatikana  katika chumba chake cha kulala  na inashukiwa aliuawa na  watu waliomkata shingoni na kutoroka .
  •  Kumekuwa na ongezeko la visa vya mauaji katika eneo hilo ambavyo chanzo chake hakijulikani 

Polisi huko Laikipia wanachunguza tukio la mauaji ya mwanamke mwenye umri wamiaka 43 katika  kijiji cha Ngobit . Mwili wake ulipatikana  katika chumba chake cha kulala  na inashukiwa aliuawa na  watu waliomkata shingoni na kutoroka .

 Kisu kilichokuwa na damu kimepatikana  kando ya mwili wake  .mwanamke huyo alikuwa akiishi karibu na baa moja ambako alikuwa akifanya kazi .Makachero  wanaucnguza tukio hilo wanalenga kubaini kilichosababisha mauaji yake .mwili wake umepelekwa katika hifadhi ya maiti .