Dereva mtovu kufikishwa kizimbani

Devera wa matatu aliyenaswa kwenye video akimtusi mwanamke na kuvunja kiyoo cha gari lake katika mtaa wa Kahawa West anafikishwa mahakamani hivi leo (Jumatatu) kujibu mashtaka kadhaa ya utovu wa nidhamu na uendeshaji mbaya wa gari.

Fredrick Nyamwanda alikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki baada ya video kuenea mitandaoni ikionyesha kiwango cha utovu wake wa nidhamu.  

Dereva huyo aliyetambulika kama Fredrick  Nyamwanda alikuwa akiendesha matatu inayomilikiwa na Mataara Sacco na anaonekana kwa video akimdhubutu mwanamke huyo akiendelea kurekodo video akimwambia kwamba hakuna mahali angempeleka.

Nyamwanda aligoga gari alimokuwa mwanamke huyo upande wa kushoto na hata kuvunja kiyoo cha pembeni na kuapa kutogharamia uharibifu huyo.

Maafisa wa Mataara Sacco wakishirikiana na maafisa wa polisi hata hivyo walifanikiwa kumkamata dereva huyo mtovu baada ya kutazama video hiyo mitandaoni na kuomba msamaha kwa mhasiriwa.

Nyamwanda anakabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari kiholela, kuharibu mali na utovu wa nidhamu.