Covid-19: Watu 337 wapatikana na corona,3 waaga dunia

Muhtasari
  • Wagonjwa 74 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi, huku 53 wakiwa wamepona corona
  • Pia watu 337 wamepatikana na corona na 3 kuaga dunia
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Watu 337 wamepatikana na virusi vya Corona baada ya sampuli 2,924 kupimwa katika saa24 zilizopita na kufikisha visa hivyo kuwa 109,164

Jumla ya sampuli zilizopimwa sasa ni 1,336,614.Kutoka visa hivyo 311 ni wakenya ilhali 26 ni raia wa kigeni .

Wanaume ni 198 ilhali wanawake ni 139 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa mwezi mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 85

 

Leo watu 53  wamepona ugonjwa huo na kufikisha 87,623 idadi ya waliopona Corona hadi sasa.

Watu 3 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 1,879ya watu waliofariki kutokana na corona.

Kuna wagonjwa 532 waliolazwa hospitalini kote nchini huku 1,498 wakiwa chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .Wagonjwa 74wapo ICU, amesema waziri wa afya MUtahi Kagwe.