Misa ya wafu ya Magufuli: Hisia kali zamzonga mama Janet Magufuli

Muhtasari

• Janet ambaye alikuwa ameketi karibu na Rais wa Tanzania Saumu Suluhu alionekana akilia bila kudhibitiwa huku akibubujikwa na machozi.

Mjane wa hayati rais Pombe Magufuli, Janet Magufuli azidiwa na hisia wakati wa misa ya wafu ya mwendake mumuwe.
Mjane wa hayati rais Pombe Magufuli, Janet Magufuli azidiwa na hisia wakati wa misa ya wafu ya mwendake mumuwe.

Mjane wa hayati John pombe Magufuli -Janet Magufuli siku ya Jumatatu alizidiwa na hisia wakati mwili wa mumuwe ulifika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa mazishi ya serikali.

Janet ambaye alikuwa ameketi karibu na Rais wa Tanzania Saumu Suluhu alionekana akilia bila kudhibitiwa huku akibubujikwa na machozi.

Janet, aliyevaa nguo nyeusi, alionekana akifarijiwa kwenye jukwaa kuu hata wakati mwili wa mumewe ulipowasili.

Umati uliposimama kuupokea mwili, Janet hakuweza kuhimili akalia hata zaidi huku akifuta machozi yake kwa leso jeupe.

Alibaki ameketi wakati wa wimbo wa Afrika Mashariki ulipokuwa ukichezwa.

Rais Suluhu alionekana akinyoosha mkono wake kuelekea kwa Janet alipojaribu kumfariji bila mafanikio.

Wanawake wawili ambao walikuwa kando ya Janet wakijaribu kumfariji pia walionekana wakijaribu kuzuia machozi.

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa nchi ambao wako Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri kwa misa ya wafu ya ya Magufuli.