Mtihani wa KCPE wang'oa nanga

Muhtasari

Takriban wanafunzi milioni 1.2 kote nchini wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE.

Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia akizindua zoezi la kusambaza mitihani ya KCPE katika kaunti ya Kisumu Machi 22
Afisa mkuu mtendaji wa TSC Nancy Macharia akizindua zoezi la kusambaza mitihani ya KCPE katika kaunti ya Kisumu Machi 22
Image: FAY MATETE

Takriban wanafunzi milioni 1.2 kote nchini wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE.

Wanafunzi hao walifanya maandalizi ya mtihani huo siku ya Ijumaa tarehe 19 Machi.

Mtihani unatarajiwa kundelea hadi Jumatano Machi 24.

 

Afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuajiri walimu (TSC) Nancy Macharia aliongoza zoezi la kuzinduliwa kwa mitihani hiyo katika kaunti ya Kisumu.

Macharia alitoa wito kwa walimu na maafisa wanaosimamia mitihani hiyo kuzingatia kanuni  za wizara ya afya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. 

 

Leo Jumatatu watahiniwa watafanya somo la Hisabati, Kiingereza Lugha na Insha ya kiingereza.

Siku ya Jumanne watahiniwa wataanza na somo la Sayansi, kisha Kiswahili Lugha na kumaliza siku kwa somo la Kiswahili Insha.

Watahiniwa wanajiandaa kwa mthani wa KCPE/ Maktaba
Watahiniwa wanajiandaa kwa mthani wa KCPE/ Maktaba
Image: EZEKIEL AMING'A

Watahiniwa watakunja jamvi la mtihani wa KCPE siku ya Jumatano kwa m

kufanya mtihani wa Somo la Jamii (Social Studies) na dini.

Wizara ya elimu ililazimika kufanyia marekebisho ratiba ya mitihani ya kitaifa na hata ratiba ya mihula kutokana na janga la covid-19.

 

Shule zilifungwa kwa takriban mwaka mzima kwa hofu ya maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa wanafunzi.

Baada ya kumaliza mtihani, wanafunzi wa darasa la nane hata hivyo watalazimika kusubiri hadi mwezi Julai kaba ya kujiunga na vidato vya kwanza.