Mahojiano ya kumtafuta jaji mkuu yaanza leo

Muhtasari

• Jumla ya wagombeaji 10 wanafuta nafasi ya kujaza pengo lililowachwa na aliyekuwa jaji mkuu David Maraga aliyestaafu.  

• Tume ya Huduma za Mahakama inachagua jina moja kwa uhakiki na idhini ya Bunge. Ikiwa imeidhinishwa Rais hufanya uteuzi rasmi.

supreme.court
supreme.court

Mahojiano ya kumsaka Jaji mkuu nchini ambaye pia atakuwa rais wa mahakama ya uoeo yameanza leo Jumatatu.

Jumla ya wagombeaji 10 wanafuta nafasi ya kujaza pengo lililowachwa na aliyekuwa jaji mkuu David Maraga aliyestaafu.  

Jaji Mkuu anateuliwa rasmi na Rais lakini anachaguliwa na Tume ya Huduma za Mahakama katika mchakato wa ushindani na mahojiano. Jaji mkuu lazima awe amehudumu kwa angalau miaka 15 kama mwanasheria.

Tume ya Huduma za Mahakama inachagua jina moja kwa uhakiki na idhini ya Bunge. Ikiwa imeidhinishwa Rais hufanya uteuzi rasmi.

WAGOMBEAJI

JAJI JUMA CHITEMBWE

Jaji Said Juma Chitembwe Picha: MAKTABA
Jaji Said Juma Chitembwe Picha: MAKTABA

Jaji Chitembwe, 54, ambaye atakuwa wa kwanza kujitosa mbele ya msasa leo Jumatatu, ana uzoefu wa miaka 29 katika taaluma ya sheria.

Anahudumu katika mahakama kuu ya Milimani; aliteuliwa jaji wa Mahakama Kuu miaka 12 iliyopita.

Kabla ya kuhamishiwa Nairobi, Chitembwe aliwahi kuwa jaji katika kaunti za Kakamega, Malindi, Marsabit na Migori.

Alifanya kazi katika shirika la NSSF kama katibu wa shirika hilo kutoka 2003 hadi 2009 kabla ya kujiunga na Mahakama.

 

Yeye ndiye mmiliki wa kampuni ya uakili ya Said Chitembwe & Co Advocates iliyoanzishwa mwaka 1994 na alifanya kazi huko hadi alipojiunga na NSSF.

Chitembwe alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 1990 na shahada ya uanasheria na alijiunga na Shule ya Sheria ya Kenya mwaka 1991.

Ana shahada ya uzamili katika Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Essex ambapo alihitimu mwaka 1994.

Kwa sasa anasomea shahada ya uzamifu (PhD) katika mafunzo amani na utatuzi wa migogoro katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro.

Wengine wanaotafuta nafasi hiyo ni kama ifuatavyo:

Prof. Kameri Mbote

Jaji Martha Koome

Jaji David Marete Njagi

Wakili Phillip Murgor

Jaji Nduma Nderi

Wakili Fred Ngatia

Jaji William Ouko

Prof. Moni Wekesa

Wakili Alice Jepkoeach Yano