Kitendawili cha mama aliyeuawa kinyama na deni la milioni 1.9

Muhtasari

• Upasuaji wa mwili ulionyesha kwamba alikuwa amenyongwa na uso wake uligongwa mara kadhaa na kifaa butu.

• Baada ya jitihada zaidi, familia ilifanikiwa kupata mawasiliano ya aliyekuwa akimdai na kubaini kuwa alikuwa ana deni la Shilingi milioni 1.9.

Milka Chemutai Rono.
Milka Chemutai Rono.
Image: HISANI

TAARIFA YA GORDON OSEN 

Wakati Milka Chemutai Rono alipoiambia familia yake mnamo Januari 7 kwamba alikuwa na deni kubwa ambalo alikuwa akihangaika kulipa, hawakujua kwamba atapoteza maisha yake muda mfupi baadaye, labda kuhusiana na deni hilo.

Mwili wake uliokuwa umeharibika vibaya ulipatikana katika ukingo wa mto katika eneo la Msitu wa Burnt Forest huko Eldoret.

Uso wa Chemutai ulikuwa umeharibika kiasi cha kutotambuka, mkono wake wa kulia ulikatwa na kidole gumba cha kushoto kilivunjwa. Alikuwa na miaka 29 na mama wa mtoto mmoja.

Familia yake ilimzika mnamo Machi 26 licha ya wingu la siri kuzunguka kifo chake.

Alikuwa akiishi na kufanya kazi katika mji wa Eldoret maisha yake yote baada ya shule ya upili.

 Nyumbani kwao eneo la Burnt Forest Januari 7, aliunda picha ya mtu alizongwa na na kufadhaishwa na mzigo wa deni, kaka yake Ignatius Kimeli aliiambia meza yetu ya habari.

Chemutai kwa ujumla alikuwa mtu mnyamavu na ilichukua juhudi kubwa kumfanya aeleze kuhusu maisha yake.

Familia ilijaribu kujua ni nani alikuwa akimdai na kiasi gani achokuwa akidaiwa, bila mafanikio mengi.

Walimshirikisha mchungaji wao wa karibu kujaribu kupata habari kutoka kwake, tena bila mafanikio.

Baada ya jitihada zaidi, familia ilifanikiwa kupata mawasiliano ya aliyekuwa akimdai na kubaini kuwa alikuwa ana deni la Shilingi milioni 1.9.

Baadaye iliibuka kuwa aliyemdai alikuwa afisa mkuu wa polisi katika mji huo.

Inashukiwa kuwa mama wa mtoto mmoja alikuwa na uhusiano na afisa huyo na baada ya kupewa pesa hizo, alitoweka.

Mnamo Januari 14, Chemutai aliondoka nyumbani, akisema kwamba alikuwa akienda Eldoret kutoa taarifa ya M-Pesa kuonyesha njia ya pesa zilivyolipwa.

Hakuonekana tena hadi Machi 20 wakati mwili wake ulipatikana ukiwa umeanza kuoza mtoni.

Kimeli alisema mara tu dada yake alipomaliza shule ya upili, alienda kukaa katika mji wa Eldoret kama mhudumu katika mkahawa.

Aliporudi miaka miwili baadaye, alisema kuwa kuna mtu alikuwa akimpangia kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret.

Hakuna chochote kilichoibuka kutoka kwake na aliishi maisha ya kawaida, akituma pesa kwa wazazi mara moja moja, alisema.

Baada ya kutoweka kwake, juhudi zilifanywa na mchungaji na familia kukutana na yule aliyemdai kupata vile angelipwa pesa zake.

"Mkutano haukufanyika huku jamaa huyo akishinda akidili msimamo kila wakati. Sharti lake lilikuwa kukutana na Milka," Kimeli alisema, akielezea kuwa aliyedai alikataa kuhudhuria mkutano bila kuwepo kwa Chemutai.

Alisema familia ilikuwa tayari kushauriana na jamaa huyo ili kufanya mipango ya kumaliza deni hilo na kuokoa maisha ya Chemutai.

Upasuaji wa mwili ulionyesha kwamba alikuwa amenyongwa na uso wake uligongwa mara kadhaa na kifaa butu.