Ripoti ya kamati maalum yataja dosari katika muswada wa BBI

Muhtasari

• Kamati hiyo ilisema, kwa mfano, pendekezo la kugawa  maeneo bunge mapya 70 kati ya kaunti 28 ni kinyume cha katiba na linataka kunyakua mamlaka ya tume ya  IEBC. 

Kamati maalum ya bunge imeashiria kile inachokiita ukiukaji sheria katika Muswada wa BBI, na kuwapa wakosoaji wake sababu mpya kupinga kura ya maamuzi.

Katika hatua ya ujasiri, Kamati ya Pamoja ya Bunge ya Haki na Kamati ya Maswala ya Sheria ilitoa uamuzi mkali kuhusu vifungu kadhaa, haswa kuundwa kwa maeneo bunge 70 mapya, na kutaja kuwa ni kinyume cha katiba.

Ajabu ni kwamba, wanachama wengi wa kamati hiyo ni washirika wa karibu wa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga, vio9ngozi wawili wa 'Handshake'  ambao ndio waanzilishi wa mikakati ya kuleta uiano.

 
 
 
 

Uhuru na wandani wake waliwaweka kando washirika wa Naibu Rais William Ruto, lakini hata Jubilee na washirika wao sasa hawakukubaliana na mambo makuu ya Muswada wa BBI.

 

Lakini licha ya ukiukwaji wa sheria, kamati hiyo ilipendekeza kwa bunge kupitisha Muswada huo na sheria zingine ambazo zinawezesha marekebisho hayo.

Kamati hiyo ilisema, kwa mfano, pendekezo la kugawa  maeneo bunge mapya 70 kati ya kaunti 28 ni kinyume cha katiba na linataka kunyakua mamlaka ya tume ya  IEBC. 

Kwa kuongezea, kamati ilikosoa pendekezo la kukomesha uhakiki wa mawaziri, Makatibu Wakuu na Makatibu wa Baraza la Mawaziri na Bunge.

 Kamati hiyo ya  pamoja iliyoongozwa na maseneta Okong’o Omogeni (Nyamira) na Kigano Muturi (Kangema) pia ililaumu pendekezo la kupunguza mamlaka ya Tume ya Huduma za Polisi  kumpa mamlaka rais,  Inspekta Jenerali wa Polisi ateuliwe na Rais.