Covid-19: Watu 5 waaga dunia,292 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 494 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,428 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 166,876  kutoka kwa sampuli 1,763,274
  • Katika visa hivi vipya, 481 ni raia wa Kenya huku 13 wakiwa raia wa kigeni, 332 ni wa kiume na 162 ni wanawake

Kenya imerekodi visa 494 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,428 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 166,876  kutoka kwa sampuli 1,763,274

Katika visa hivi vipya, 481 ni raia wa Kenya huku 13 wakiwa raia wa kigeni, 332 ni wa kiume na 162 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 50 wamepona virusi vya corona,27  walipona wakiwa nyumbani huku 23  wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 114,285 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 5 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,040 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,085 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,624 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 109 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).