Covid-19:Watu 1,437 wapona corona,31 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 619 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,647 chini ya saa 24 zilizopita
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 229,628  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.3%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imesajili visa 619 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,647 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 229,628  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.3%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 606 ni wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni,308 ni wanaume huku 311 wakiwa wanawake.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,31,674.

Kati ya maambukizi hayo mapya, kaunti ya Nairobi imeongeza kwa visa 247, Kiambu ina visa 166 huku Nakuru ikiwa na visa 30.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 3, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 94.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 31 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,528 ya walioaga dunia.

Aidha watu 1,437 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 213,473, 1,318 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 119 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa2,004 ambao wamelazwa hospitalini,8,292wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 170 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).