Mwanamke aliyemshtaki spika Ken Lusaka kwa kuruka mimba atupilia mbali kesi hiyo

Muhtasari
  • Mwanamke aliyemshtaki spika Ken Lusaka kwa kuruka mimba atupilia mbali kesi hiyo
Spika wa Seneti Ken Lusaka. Picha: HISANI
Spika wa Seneti Ken Lusaka. Picha: HISANI

Afueni kwa Spika wa Bunge la Seneti Kenneth Lusaka baada ya mwanamke aliyemshataki kwa ajili ya uzazi na ulezi wa mtoto kuondoa kesi hiyo.

Hii ni baada ya mwanamke huyo kuondoa kesi aliyowasilisha dhidi ya spika kufuatia mikutano kadhaa kati yapande zote mbili.

Kupitia wakili Danstan Omari, mwanamke huyo anasema hatafuatilia kesi hiyo ambayo aliwasilisha kortini.

"Kumbuka kuwa mwombaji ameondoa kabisa kesi  yote ya Juni 15 2021 pamoja na maombi yote ya kuhudhuria," inasomeka ilani ya kujitoa.

Wakili Omari amekataa kufichua makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mteja wake na Lusaka.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu alihamia kortini kumshtaki spika kwa kumtelekeza yeye na mtoto ambaye hajazaliwa.

Alitaka spika alazimishwe kuunga mkono utunzaji wake kabla ya kuzaa, matengenezo akisema kwamba alikuwa mtu wa hali ya juu.

Kulingana na mwanamke huyo, Sh25 Milioni zingetosha kumtunza mtoto kabla na baada ya kuzaliwa.