COVID 19: Watu 1, 045, 918 wamechanjwa kikamilifu nchini, Kiwango cha maambukizi ni 3.9%

Muhtasari

•Kufikia sasa Kenya imewahi kurekodi visa 251, 057 kutoka kwa jumla ya vipimo 2, 602, 818 ambavyo vimewahi kufanywa tangu mwanzo wa janga la Corona.

MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Wizara ya afya imetangaza visa vipya  159 nchini kutoka kwa sampuli ya watu 4,406 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita. Hii inaashiria kwamba asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 3.9%.

Kufikia sasa Kenya imewahi kurekodi visa 251, 057 kutoka kwa jumla ya vipimo 2, 602, 818 ambavyo vimewahi kufanywa tangu mwanzo wa janga la Corona.

Nairobi imeripoti visa 28, Meru 17, Turkana 12, Makueni 11, Bungoma 10 huku kaunti zingine zikiandikisha visa chini ya kumi.

Wagonjwa 181 wameweza kupona, 177 wakiponea nyumbani huku 64 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 243, 772 wamewahi kupona maradhi hayo.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 5181 baada ya vifo 2 zaidi kuripotiwa leo.

Kwa sasa wagonjwa 789  wanahudumiwa hospitalini huku wengine 1809 wakipokea matibabu kutoka manyumbani kwao. Wagonjwa 48 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa watu 3,126, 284 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 1, 045, 918 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.