Ethiopia yatangaza hali ya hatari

Muhtasari

• Serikali awali ilikuwa imewataka wakaazi katika mji mkuu wa Addis Ababa kujihami , huku waasi kutoka kaskazini mwa Tigray wakisonga mbele kuelekea eneo la kusini.

Wapiganaji wa Tigray wamefanikiwa kudhibiti maeneo mengi ya jimbo hilo tangu mwezi Juni
Wapiganaji wa Tigray wamefanikiwa kudhibiti maeneo mengi ya jimbo hilo tangu mwezi Juni
Image: GETTY IMAGES

Serikali ya Ethiopia imetangza hali ya hatari huku vita vikienea katika majimbo kadhaa nchini humo.

Serikali awali ilikuwa imewataka wakaazi katika mji mkuu wa Addis Ababa kujihami , huku waasi kutoka kaskazini mwa Tigray wakisonga mbele kuelekea eneo la kusini.

Kituo cha habari , Addis Stabdard , kimeripoti kwamba waziri wa haki amezungumzia kuhusu tangazo hilo la hali ya tahadhari.