Makali ya corona:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,959,988,177 wapona

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 25 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni,15 ni wanaume huku 13 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,979 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.9%
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Watu 28 wamepatatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,969 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 25 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni,15 ni wanaume huku 13 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,979 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,830,071.

Aidha watu 177 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 248,308,154 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 23 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Mtu 1 ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,334.

Kuna wagonjwa 169 ambao wamelazwa hospitalini, 816 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 7 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,959,988.