(Picha) Licha ya mvua maelfu wajitokeza kwa hafla ya Raila Kasarani

Muhtasari

• Raila anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuania urais ambapo atakuwa anajaribu kutafuta kiti hicho kwa mara ya sita.

Licha ya kibaridi kikali na manyunyu maelfu ya wafuasi wa kinara wa upinzani Raila Odinga wamejitokeza katika uwanja wa Kasarani jijini Narobi kwa hafla yake maalum.

Raila anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuania urais ambapo atakuwa anajaribu kutafuta kiti hicho kwa mara ya sita.

Viongozi kadhaa mashuhuri tayari wamewasili katika uwanja huo.