Matiang’i aagiza machifu na manaibu wa Nyanza kupeana vitambulisho ambavyo havijachukuliwa

Muhtasari

•Machifu na manaibu wameagizwa kuhakikisha vitambulisho hivyo ambazo vimesalia vimepewa wenyewe kabla ya januari.

•Aliendelea kueleza machifu ni wajibu wao kuhakikisha vijana ambao wamefikisha umri wa kupata vitambulisho wamewasaidia kuzipata kwa njia rahi

Waziri Fred Matiang'i
Waziri Fred Matiang'i
Image: Ezekiel Aming'a

Waziri wa usalama wa ndani Fred matian’gi alhamisi alieleza takribani vitambulisho 52,000 ziko katika ofisi kuu za kaunti .

Machifu na manaibu wameagizwa kuhakikisha vitambulisho hivyo ambazo vimesalia vimepewa wenyewe kabla ya januari.

Alieleza kwamba ifikiapo Januari usajiri wa wapiga kura utangoa nanga katika maneo yote ya usajiri na kitambulisho ni moja yapo ya mahitaji.

“Tutaanza kuandikisha tena wapiga kura kuanzia mwezi wa januari, Nyanza Province sisi wenyewe tuko na ID card 52,000 ambazo hazijachukuliwa kutoka kwa ofisi kuu za kaunti” alisema Matiang’i

Aliendelea kueleza machifu ni wajibu wao kuhakikisha vijana ambao wamefikisha umri wa kupata vitambulisho wamewasaidia kuzipata kwa njia rahisi.

“Ni kazi yetu sisi machifu na naibu kupita pande zote. Na mimi nataka kamisna wa kaunti, kwa sababu wao wako hapa na hivi karibuni tutazunguza.  Hawa vijana wataweza kujisajiri vipi bila vitambulisho” Alisema.

Vilevile aliwakumbusha njia ambazo wanapaswa kufuata wakati wa uchaguzi mkuu 2022 kama Rais alivyosema

“Na Rais wetu akituagiza twende pande hii kama kiongozi, tunafuata huo mtindo. Alafu mtu aniambie hio sio demokrasia. Nchi inaongozwa na utaratibu ama namna gani?” Matiang'i alisema.