DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi

Muhtasari
  • DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi
  • Wiki iliyopita, ANC ilikanusha ripoti kwamba imemwalika Ruto kwenye uzinduzi wa azma ya urais ya Mudavadi
DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi
Image: Ezekiel Aming'a

Naibu rais William Ruto amewasili katika mkutano wa  kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi wa kutangaza azma yake ya kuwania urais.

Ruto aliwasili akiwa ameandamana na viongozi wa UDA akiwemo Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, Mbunge wa Garissa mjini Aden Duale, Kimani Ichungwa miongoni mwa wengine.

Alifika saa 2 jioni huku umati wa watu ukimpokea kwa mbwembwe.

Miongoni mwa waliohudhuria ni seneta wa Murang'a Irungu Kang'ata, Nelson Havi wa LSK, Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa miongoni mwa wengine.

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa katika ukumbi huo pia alijitokeza katika hali isiyoeleweka.

Musalia Mudavadi na naibu rais William Ruto
Image: Andrew Kasuku

Wiki iliyopita, ANC ilikanusha ripoti kwamba imemwalika Ruto kwenye uzinduzi wa azma ya urais ya Mudavadi.

Mnamo Alhamisi, seneta mteule Petronila Were aliambia Star kwamba Ruto hajaalikwa kwenye Bomas of Kenya Jumapili.

"Uongozi wa juu wa kisiasa wa nchi ambao tumealika ni wakuu wa Oka, naweza kuthibitisha hilo kwa sababu nilitia saini barua," Were alisema.

Aliendelea, "Zilizosalia ni uvumi tu kwa sababu kiongozi mwingine tuliyemwalika ni spika Muturi ambaye ni rafiki wa kibinafsi wa kiongozi wetu wa chama."

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala pia alisema Ruto na maafisa wa UDA hawakuwa wamealikwa kwenye kongamano hilo.

DP Ruto awasili Bomas katika uzinduzi wa azma ya urais wa Mudavadi
Image: Ezekiel Aming'a