Joyce Ngugi kuwania ubunge Gatundu kusini

Muhtasari

• Naibu gavana kaunti ya Kiambu, Joyce Ngugi ametangaza rasmi kwamba atakuwa anawania kiti cha ubunge katika eneo la Gatundu kusini katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

• Ikumbukwe kwamba Ngugi aliwania ubunge wa Gatundu katika chaguzi za mwaka wa 2017 ila akabwagwa na Moses Kuria, huku mwaka huu akipania kutoana kijasho na wapinzani wengine sita.

 

Joyce Ngugi
Joyce Ngugi
Image: KWA HISANI

Naibu gavana kaunti ya Kiambu, Joyce Ngugi ametangaza rasmi kwamba atakuwa anawania kiti cha ubunge katika eneo la Gatundu kusini katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Ngugi amechukua nafasi hiyo kumshukuru rais Uhuru Kenyatta kwa maendeleo ambayo ameleta katika eneo hilo kwa ushirikiano na mbunge wa sasa, Moses Kuria.

Akizungumza na vyombo vya habari, naibu gavana huyo amesema kwamba wakazi wa eneo hilo wamempa Baraka na kumruhusu kuzuru kona zote za eneo bunge la Gatundu kusini  ili kuomba kura na kuuza sera zake kwa wananchi.

Ikumbukwe kwamba Ngugi aliwania ubunge wa Gatundu katika chaguzi za mwaka wa 2017 ila akabwagwa na Moses Kuria, huku mwaka huu akipania kutoana kijasho na wapinzani wengine sita.

Aidha amemtakia afueni ya haraka mbunge wa sasa Mose Kuria ambaye anaendelea kupata matibabu katika taifa la Dubai na kumshukuru kwa jinsi ambavyo amepambana kuhakikisha wakazi wanapata maisha mazuri.