Covid-19:Visa 32 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa,28 wapona

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 24 ni wakenya huku 8 wakiwa raia wa kigeni,25 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 323,057 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.5%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Watu 32 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 6,528 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 24 ni wakenya huku 8 wakiwa raia wa kigeni,25 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 323,057 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,393,571.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miaka 12, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 72.

Vile vile watu 28 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 303,324, 22 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 6 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Hamna mtu ameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,640.

Kuna wagonjwa 39 ambao wamelazwa hospitalini 477 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna mgonjwa 1 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 16,829,500.