Bodaboda wote watasajiliwa upya - Uhuru

Muhtasari
  • Akizungumza siku ya Jumanne, Mkuu wa Nchi pia aliagiza msako mkali dhidi ya waendesha bodaboda wote walaghai kote nchini

Rais Uhuru Kenyatta ameamuru waendeshaji bodaboda wote kusajiliwa upya.

Akizungumza siku ya Jumanne, Mkuu wa Nchi pia aliagiza msako mkali dhidi ya waendesha bodaboda wote walaghai kote nchini.

Aliwaonya viongozi dhidi ya kuingiza siasa katika suala hilo.

Mkuu wa nchi alikuwa akijibu video moja kwa moja ambapo dereva wa kike alinyanyaswa kingono katika Barabara ya Wangari Maathai jijini Nairobi mnamo Ijumaa, wiki iliyopita.

Kulingana na rais, video hiyo "ilivunja moyo" kuona.

Alikuwa akizungumza katika Shule ya Serikali ya Kenya iliyoko Lower Kabete ambako alikuwa mgeni mkuu katika sherehe za kitaifa za Siku ya Kimataifa ya Wanawake mwaka huu.

“Tutawasajili tena nyote na lazima tuhakikishe kuwa tunawalinda wanawake. Nimewaagiza maafisa wa kutekeleza sheria kutumia vyombo vilivyo ndani ya sheria kuwaadhibu wahusika hawa

Hatupaswi kuwa na marudio ya kile tulichoona,"Rais alizungumza.

Vile vile Rais aliwaonya wanasiasa dhidi ya kujihusisha na ukandamizaji huo kama ajenda ya kampeni katika mikutano ya kisiasa, akisema kuwa serikali itaunga mkono waendeshaji kwa sharti kwamba wawe na nidhamu.

"Tuko katika msimu wa siasa  na kuna wengine huko ambao wataenda na kuanza kusema serikali inawanyanyasa wafanyabiashara wadogo na wafanyabiashara ... tunataka kukusaidia biashara inafanikiwa lakini lazima pia ufanye bidii yako,” alisema Kenyatta.