Wanawake wapatikana wakisafirisha gunia 6 za bangi kutoka Busia kupeleka Nairobi

Muhtasari

•Caroline Mariwa na Nancy Wangare walikamatwa Jumatatu jioni katika eneo la Saba Saba, kaunti ya Murang'a wakisafirisha mihadarati hiyo kutoka Busia kuelekea Nairobi.

•Wawili hao ambao walikuwa wanasafiri kwa gari aina ya Toyota Wish walikuwa wametia kasi kubwa  katika juhudi za kuwatoroka wapelelezi wa kitengo cha TUCO.

Image: TWITTER// DCI

Wapelelezi wa kitengo cha DCI wanawazuilia wanawake wawili kwa kosa la ulanguzi wa mihadarati aina ya bangi.

Caroline Mariwa na Nancy Wangare walikamatwa Jumatatu jioni katika eneo la Saba Saba, kaunti ya Murang'a wakisafirisha mihadarati hiyo kutoka Busia kuelekea Nairobi.

Gunia sita zilizokuwa na vifurushi vya bangi zilipatikana.

Kabla ya kukamatwa kwao, wawili hao ambao walikuwa wanasafiri kwa gari aina ya Toyota Wish walikuwa wametia kasi kubwa  katika juhudi za kuwatoroka wapelelezi wa kitengo cha TUCO.

Washukiwa walikuwa wametumia barabara ndefu ya Nakuru-Nyahururu-Nyeri-Murang'a ili kupunguza uwezekano wao kukamatwa.

Kwa sasa wanazuiliwa katika makao makuu ya DCI wakisubiri kufikishwa mahakamani.