Covid-19:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 17,244,066

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 11 ni wakenya huku 7 wakiwa raia wa kigeni,11 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 323,237 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.4%
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe
Image: Mercy Mumo

Watu 18 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 4,287 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 11 ni wakenya huku 7 wakiwa raia wa kigeni,11 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 323,237 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.4%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,457,194.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miaka 2, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 67.

Vile vile watu 4 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 317,527.

Hamna mtu ameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,647.

Kuna wagonjwa 19 ambao wamelazwa hospitalini 125 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna mgonjwa 1 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 17,244,066.

 

 

 

 

 

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe
Image: Mercy Mumo