Agizo la kukamatwa imetolewa dhidi ya Didimus Barasa kufuatia madai ya mauaji

Mbunge huyo wa Kimilili bado hajulikani aliko na simu yake imezimwa.

Muhtasari

•Haji ameagiza kukamatwa kwa mbunge huyo ili kurekodi taarifa ambayo inafaa kuwasilishwa kwa ofisi yake. 

• Barasa alipochomoa bastola na kumlenga msaidizi wa Khaemba Brian Olunga na kumpiga risasi ya paji la uso.

Kimilili MP Didmus Barasa
Kimilili MP Didmus Barasa
Image: HISANI

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji ametoa ilani ya kukamatwa kwa mbunge wa Kimilili Didimus Barasa kufuatia madai ya mauaji.

Barasa anadaiwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Brian Khaemba kufuatia ugomvi ulitokea katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi Jumanne jioni. Bw Brian Olunga na kumpiga  alifariki katika hospitali ya Kimilili Subcounty alipokuwa akipokea matibabu ya dharura.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni, Haji ameagiza kukamatwa kwa Barasa, kurekodi taarifa na faili husika kuwasilishwa ofisini kwake kwa hatua stahiki.

"Kulingana na polisi huko Bungoma, mbunge huyo bado hajulikani aliko na simu yake imezimwa," Haji alisema kupitia Twitter.

Jumanne, mkuu wa DCI wa Bungoma Joseph Ondoro alisema Barasa alizozana na Khaemba, hatua ambayo ilimfanya  mpinzani huyo wake kuondoka na kuelekea kwenye gari lake.

"Barasa alimfuata akiwa na wanaume wanne na kuwaamuru wasimruhusu (Khaemba) kuondoka mahali hapo lakini dereva wa Khaemba Joshua Nasokho alikaidi amri hiyo na kuwasha gari," alisema Ondoro.

Hapo ndipo Barasa alipochomoa bastola na kumlenga msaidizi wa Khaemba Brian Olunga na kumpiga risasi ya paji la uso.Olunga alifariki katika hospitali ya Kimilili Subcounty alipokuwa anapokea matibabu ya dharura.

Ondoro alisema wanamtafuta Barasa kwa ajili ya kuhoji kuhusu tukio hilo.

“Amekimbia lakini tunamtafuta. Ajisalimishe,” alisema.