IG Hillary Mutyambai na DCI George Kinoti wajiuzulu

Mutyambai amekuwa hospitalini akiugua na alikuwa amemteua Noor Gabow kaimu inspekta mkuu wa polisi.

Muhtasari

• Akitangaza baraza la mawaziri siku ya Jumanne Ruto alisema kwamba hatua ya Mutyambai kujiuzulu imetokana na hali yake ya kiafya.

Kinoti na Mutyambayi wajiuzulu nyadhifa zao
Kinoti na Mutyambayi wajiuzulu nyadhifa zao
Image: Maktaba

Rais William Ruto ametangaza kwamba Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai amejiuzulu.

Akitangaza baraza la mawaziri siku ya Jumanne Ruto alisema kwamba hatua ya Mutyambai kujiuzulu imetokana na hali yake ya kiafya.

Mutyambai amekuwa hospitalini akiugua na alikuwa amemteua Noor Gabow kuwa kaimu inspekta mkuu wa polisi.

Rais Ruto pia alitangaza kujiuzulu kwa mkurugenzi wa idara ya CID George Kinoti.

Ruto alikuwa mara nyingi amekosoa utendakazi wa Kinoti na inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai.