MSTAKABALI

Babu awarai wanafunzi wa kiume kufanya bidii

Babu alikuwa akiwahutubia wanafunzi wa shule za msingi kutoka eneo bunge la Nyakach.

Muhtasari

•Wanafunzi hao walikuwa wamesafiri hadi Nairobi kuzuru majengo ya Bunge la Kenya.

•Baadhi yao watakalia mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi (KCPE) mwezi ujao.

Mbunge wa Embakasi East Babu Owino
Image: Facebook// Babu Owino

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewashauri wavulana kufanya bidii shuleni ili waweze kufurahia maisha bora siku za usoni.

Mbunge huyo wa awamu ya pili aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wanafunzi wa shule za msingi kutoka eneo bunge la Nyakach.

Wanafunzi hao walikuwa wamesafiri hadi Nairobi kuzuru majengo ya Bunge la Kenya.

Baadhi yao watakalia mitihani ya Cheti cha Elimu ya Msingi (KCPE) mwezi ujao.

"Nataka ufuatilie elimu na elimu pekee. KCPE yako itafanyika. Novemba hakikisheni mnapita kwani huo ndio ufunguo wa maisha yajayo, ukifaulu uwezekano wa wewe kufanikiwa kimaisha ni mkubwa sana,” alisema Babu.

Babu aliwataka wavulana kulenga alama nzuri shuleni, akiwakumbusha kuwa mara nyingi wanaume pekee ndio huishia kutunza familia.

Kama wavulana, mnajua nyinyi ndio walezi, siku za usoni baada ya kujifunza kumaliza shule ya msingi hivi karibuni, nenda sekondari na kisha chuo kikuu, mwishowe utapata fami. kwa kweli, ninyi kama wavulana mtakuwa walezi,” Babu alieleza.