Winnie Odinga, mwanawe Kalonzo ashinda awamu ya kwanza ya kura za EALA

Washindi wa mwisho wa nafasi nne katika kambi ya Azimio watajulikana baada ya Bunge la Kitaifa kukamilisha upigaji kura.

Muhtasari
  • Mwanawe Kalonzo Kennedy Musyoka aliongoza kwa kura 45 katika kambi ya Azimio, akifuatiwa na Suleiman Shahbal aliyepata kura 38 huku Winnie Odinga akijizolea kura 35
WINNIE ODINGA
Image: KWA HISANI

Seneti imekamilisha kupiga kura kuwachagua wawakilishi wa Kenya katika Bunge la Afrika Mashariki.

Mwanawe Kalonzo Kennedy Musyoka aliongoza kwa kura 45 katika kambi ya Azimio, akifuatiwa na Suleiman Shahbal aliyepata kura 38 huku Winnie Odinga akijizolea kura 35.

Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hicho kwa upande wa wachache walipata alama zifuatazo;

Fatuma Gedi (31), Kanini Kega (29), Diriye Mohamed (4), Timothy Bosire (17), Justus Kizito (9), Jeremiah Kioni (1), Wilfred Mutua (0), Beatrice Askul (1) na Hellen Mueni (1).

"Tutawasilisha kama Bunge matokeo kwa Bunge la Kitaifa kwa njia ya ujumbe tunaposubiri matokeo kutoka kwa Bunge la Kitaifa," Spika Amason Kingi alisema.

Washindi wa mwisho wa nafasi nne katika kambi ya Azimio watajulikana baada ya Bunge la Kitaifa kukamilisha upigaji kura.

Azimio kama upande wa wachache ina nafasi nne za kujaza katika bunge la kikanda, chini ya upande wa Kenya Kwanza walio wengi.