Rais Ruto ashukuru benki na wakurugenzi wa kampuni za simu

"Si mara zote washindani huketi pamoja ili kuafikiana kuhusu bidhaa ambayo si lazima iwe yao," Ruto alisema.

Muhtasari
  • "Ninataka kuwashukuru KCB na Family Bank, wametembea nasi..na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za simu," alisema.
RAIS WILLIAM RUTO
Image: PCS

Rais William Ruto Jumatano alitaja kama kitendo cha uzalendo ushirikiano wa benki na makampuni ya simu katika kuunda Hustler Fund.

Rais alipongeza Maafisa Watendaji Wakuu wa benki -zinazozitaja KCB na Family Bank-kwa kufanya kazi na serikali yake kufanikish Hustler Fund.

Ruto ambaye alizungumza alipozindua hazina hiyo, alisema utawala wake unashukuru watoa huduma za simu kwa kujitolea kwao katika mradi huo.

"Si mara zote washindani huketi pamoja ili kuafikiana kuhusu bidhaa ambayo si lazima iwe yao," Ruto alisema.

"Kutokana na uzalendo, tumewaona wakija pamoja ili tuweze kutengeneza Hustler Fund ili kutoa nafasi kwa watu wa Kenya."

Rais alisema Wakurugenzi Wakuu wa Safaricom, Telcom na Airtel pamoja na wale wa benki walikaa naye kwa muda mrefu kuandaa hazina hiyo.

"Ninataka kuwashukuru KCB na Family Bank, wametembea nasi..na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni za simu," alisema.

"Nina furaha leo tutawakomboa Wakenya ambao walikuwa wamefungiwa nje ya mkopo kwa sababu hawakuweza kukopa."