Mwanamume auawa baada ya kaka wawili waliokuwa na uhusiano wa kipampenzi na dada yao kupigana , Kirinyaga

Wawili hao wanasemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yao mdogo mwenye umri wa miaka 17.

Muhtasari

• Wapelelezi waliofika katika eneo la mkasa waligundua kuwa marehemu alikuwa hata amedaiwa kumtunga mimba dada yao mwaka jana.

Image: DCI

Wapelelezi wanamsaka mwanamume wa umri wa miaka 31 ambaye anadaiwa kumuua kakake mkubwa katika kisa cha madai ya ugomvi wa kimapenzi unaohusisha dada yao mdogo. 

Wawili hao wanasemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yao mdogo mwenye umri wa miaka 17. 

Mshukiwa anasemekana kumpiga kakake mwenye umri wa miaka 37 kwa kutumia kifaa butu kichwani, usoni na mgongoni baada ya kumpata katika mazingira ya kutatanisha na dada yao wa kambo mwenye umri wa miaka 17. 

Idaya ya DCI ilisema kwamba ndugu hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yao wa kambo. 

"Marehemu pia alikuwa na mapenzi ya siri na msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 na hakuweza kukubaliana na kile alichokishuhudia," taarifa hiyo ilisema. 

Marehemu aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Karatina. 

Wapelelezi waliofika katika eneo la mkasa waligundua kuwa marehemu alikuwa hata amedaiwa kumtunga mimba dada yao mwaka jana, lakini alipoteza mimba hiyo mwezi Machi mwaka huu.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO