Mwanafunzi bora wa KCPE 2022 amezoa alama 431

Jumla ya wanafunzi 1, 214, 013 walikalia mtihani wa KCPE 2022.

Muhtasari

•Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC mnamo Desemba 21, 2022 mwendo wa adhuhuri.

•Wanafunzi 9443 walifanikiwa kupata alama 400 kuenda juu. 

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alipotoa matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC kando ya Barabara ya Dennis Pritt Kilimani, Nairobi mnamo Desemba 21, 2022.
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alipotoa matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC kando ya Barabara ya Dennis Pritt Kilimani, Nairobi mnamo Desemba 21, 2022.
Image: ANDREW KASUKU

Mwanafunzi bora wa KCPE 2022 alipata alama 431.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alitangaza matokeo ya KCPE katika afisi za KNEC zilizo kando ya barabara ya Dennis Pritt, mtaa wa Kilimani, Nairobi mnamo Desemba 21, 2022 mwendo wa adhuhuri.

Machogu alibainisha kuwa watahiniwa walifanya vyema katika mtihani wa mwaka huu ikilinganishwa na mtihani wa 2021 ambapo mtahiniwa bora alipata alama 428.

Takriban watahiniwa 1,244,188 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambao ulifanyika Novemba 28 hadi 30.

Wanafunzi 9443 walifanikiwa kupata alama 400 kuenda juu. Watahiniwa wengine 307, 756 walipata kati ya alama 300 na 399.

Watahiniwa 619 593 walipata alama kati ya 200 na 299 huku 296,336 wakipata alama kati ya  100 na 199. Wanafunzi 724 walipata alama 99 kuenda chini.