Kwa nini DP Gachagua anataka kuendeleza masomo yake

DP alisema ana shahada moja tu, wakati Rais ana tatu jambo ambalo linamfanya awe na ujuzi zaidi.

Muhtasari
  • Aliwataka maafisa hao wa polisi kufikiria pia kuendeleza masomo yao mara wapatapo nafasi

Mahakama yakubali ombi la kutupiliwa mbali kesi ya ufisadi dhidi ya DP Gachagua.
Mahakama yakubali ombi la kutupiliwa mbali kesi ya ufisadi dhidi ya DP Gachagua.
Image: Facebook//RigathiGachagua

Naibu Rais Rigathi Gachagua amemwomba Rais William Ruto amruhusu kuendeleza masomo yake mara tu mzigo wa kazi ofisini utakapopungua.

DP alisema ana shahada moja tu, wakati Rais ana tatu jambo ambalo linamfanya awe na ujuzi zaidi.

Gachagua alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Kitaifa cha Uongozi wa Huduma ya Polisi huko Ngong, kaunti ya Kajiado.

"Your Excellency ata masomo yangu ni kidogo, utanipatia ruhusa kazi ikipungua niongeze kidogo," Alisema.

Alisema wakati mwingine huhisi changamoto wanapohudhuria mikutano.

"Kwa hile kazi nimepewa na rais, masomo yangu iko chini kidogo, unajua mimi niko na degree moja, my boss has three, si unaona  hio kibarua ni kali. Tena one of my senior colleague ni professor, so pale kwa mikutano saa zingine ua ninachanganikiwa." 

Aliwataka maafisa hao wa polisi kufikiria pia kuendeleza masomo yao mara wapatapo nafasi.

DP alisema Chuo cha Uongozi hakingekuja kwa wakati mzuri zaidi, kwani kingetoa ujuzi muhimu wa uongozi kwa makamanda wa polisi ili kuongeza utoaji wa huduma katika huduma ya polisi.