Mshukiwa mkuu Jackton Odhiambo akiri kumuua mwanamitindo Chiloba

Mshukiwa huyo anasema alimuua Chiloba kama kulipiza kisasi kwa kumsaliti katika uhusiano wao.

Muhtasari
  • Na kulingana na maneno yake, Odhiambo aliihama nyumba hiyo mara moja
MWANAHARAKATI EDWIN CHILOBA
Image: HISANI

Jackton Odhiambo, mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanamitindo Edwin Chiloba amekiri kumuua mwanamitindo huyo kwa madai kwamba alimsaliti.

Kulingana na OCPD wa Langas John Odhiambo, Jackton alitekeleza mauaji hayo kwa usaidizi wa marafiki zake wawili ambao bado hawajapatikana.

Mshukiwa huyo anasema alimuua Chiloba kama kulipiza kisasi kwa kumsaliti katika uhusiano wao.

Odhiambo ambaye alikuwa amekaa na marehemu kwa muda wa mwaka mmoja mjini Eldoret alikamatwa Ijumaa akiwa mshukiwa mkuu wa mauaji hayo.

Wawili hao walikuwa wakiishi pamoja kama mume na mke.

Msimamizi wanyumba alikoishi wa Chiloba Alex Nyamwea anasema kwamba Jackton Odhiambo alimpigia simu akitumia simu ya Chiloba mnamo Januari 4 akimjulisha kwamba alikuwa akihama nyumba waliyokuwa wakiishi.

Na kulingana na maneno yake, Odhiambo aliihama nyumba hiyo mara moja.

Polisi wanachunguza uwezekano wa kuhusishwa na mapenzi baada ya mshukiwa mkuu Jackton Odhiambo kukiri kwamba alifukuzwa kutekeleza mauaji hayo baada ya kubaini kuwa Chiloba alikuwa na mpenzi mwingine.