- OCPD wa Marakwet Magharibi Bosita Omulongolo alithibitisha shambulio lililosababisha kuuawa kwa fundi wa maabara
Maafisa wawili wa afya wameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi huko Kerio Valley licha ya operesheni inayoendelea ya KDF kuungwa mkono na usalama.
Gavana wa Elgeyo Marakwet Wisley Rotich ameelezea kughadhabishwa na mauaji hayo na kusema kuwa idadi ya waliofariki kutokana na mashambulizi ya hivi punde imeongezeka hadi watano ndani ya siku nne.
Muuguzi wa kike katika hospitali ya misheni ya Endo aliuawa alipokuwa akielekea kazini huku fundi wa maabara aliyekuwa akichunga wanyama wake akipigwa risasi na kufa huko Arror.
Wahasiriwa hao wawili wote wana umri wa makamo.
Katika chapisho la mtandao wa kijamii, Rotich alitangaza kwamba inatosha na kwamba wangeanza kuzipa jamii silaha katika eneo hilo kwa ajili ya kujilinda.
"Tutaanza kuwapa watu silaha kuanzia Jumatatu ikiwa KDF na polisi hawatachukua hatua kufikia wakati huo," Rotich alisema.
Hofu imetanda katika eneo hilo kufuatia mashambulizi ya hivi punde...
OCPD wa Marakwet Magharibi Bosita Omulongolo alithibitisha shambulio lililosababisha kuuawa kwa fundi wa maabara.
Polisi huko Marakwet Mashariki wametumwa kuwasaka waliomshambulia muuguzi huyo