Watalii wawili wa kigeni wafariki katika ajali ya Maasai Mara nchini Kenya

Mtalii mwingine mmoja alijeruhiwa na wengine wawili kulinusurika bila majeraha.

Muhtasari

• Hifadhi ya taifa ya Maasai Mara ni kivutio maarufu cha utalii kwa wenyeji na wageni.

Gari lao lilikwama na kupoteza mwelekeo (picha ya faili)
Gari lao lilikwama na kupoteza mwelekeo (picha ya faili)
Image: Getty Images

Watalii wawili wa kigeni, Mjerumani na Mswizi, walifariki katika ajali katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara nchini Kenya siku ya Jumamosi.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari walilokuwa wakitumia kwa ziara yao kukwama na kupoteza mwelekeo, polisi walisema.

Gari hilo lilikuwa limebeba raia watatu wa Ujerumani na wawili wa Uswizi, wakati ajali hiyo ilipotokea kando ya daraja la Sekenani-Mara.

Mtalii mwingine mmoja alijeruhiwa na wengine wawili walinusurika bila majeraha. Mtalii aliyejeruhiwa alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, vyombo vya habari vya ndani vilisema.

Polisi wa Kenya walisema ajali hiyo inachunguzwa.

Hifadhi ya taifa ya Maasai Mara ni kivutio maarufu cha utalii kwa wenyeji na wageni.