Watu 7 zaidi waokolewa kutoka dhehebu potovu Malindi, huku muhubiri akisubiri kufikishwa mahakamani

Katika kituo cha polisi cha Malindi, wanafamilia wa waathiriwa wa Mackenzie walikusanyika wakiwa na matumaini ya kuwapata jamaa zao.

Muhtasari
  • Mnamo Aprili 14, wafuasi wanne wa ibada hiyo, ambao walidaiwa kulaghaiwa kufunga na Mackenzie walikufa. Wengine 11 walilazwa hospitalini.
Crime Scene
Image: HISANI

Wafuasi wengine saba wa dini ya kustaajibisha katika kijiji cha Shakahola, eneo la Malindi, kaunti ya Kilifi wameokolewa.

Saba hao waliokolewa Jumapili usiku katika juhudi zilizowekwa na MCA Wa Adu Samason Zia Kahindi, ambaye aliwapeleka hadi kituo cha Polisi cha Malindi.

Haya yanajiri huku mhubiri Paul Mackenzie Nthenge wa kanisa la Good News International Church anayesemekana kuongoza ibada hiyo akisubiri kufikishwa mahakamani katika mahakama kuu ya Malindi.

Polisi wataomba kupewa muda zaidi wa kumzuilia Mackenzie huku wakikusanya ushahidi zaidi dhidi yake kwa kuongoza ibada inayofanana na ya kidini, ambapo waabudu hufunga hadi "ili waweze kumuona Mungu".

Mnamo Aprili 14, wafuasi wanne wa ibada hiyo, ambao walidaiwa kulaghaiwa kufunga na Mackenzie walikufa. Wengine 11 walilazwa hospitalini.

Katika kituo cha polisi cha Malindi, wanafamilia wa waathiriwa wa Mackenzie walikusanyika wakiwa na matumaini ya kuwapata jamaa zao.

Wengine walisema kuwa wamewaona jamaa zao kwenye vyombo vya habari baada ya kuokolewa lakini walikuwa bado hawajaonana nao.

Familia hizo zilisafiri kutoka maeneo ya mbali  huku wengine wakiwa wakazi wa Kaunti ya Kilifi.