Wacheni kuwakamata vijana wanaokunywa pombe-Raila amsuta Gachagua

Raila Odinga alimweleza Rigathi Gachagua kuwa ikiwa anataka vijana wakome unywaji pombe basi awape kazi.

Muhtasari
  • Hivi majuzi Rigathi Gachagua alizindua msako dhidi ya pombe haramu ambayo inanuiwa kukomesha kizazi cha vijana katika eneo la Mlima Kenya.
Ruto aapa kuendelea kumuita Odinga "my brother" ili kumaliza maandamano
Ruto aapa kuendelea kumuita Odinga "my brother" ili kumaliza maandamano
Image: Facebook

Aliyekuwa waziri mkuu Mh Raila Odinga ametoa onyo kali kwa naibu rais Rigathi Gachagua baada ya kuwakamata vijana wanaokunywa pombe.

Hivi majuzi Rigathi Gachagua alizindua msako dhidi ya pombe haramu ambayo inanuiwa kukomesha kizazi cha vijana katika eneo la Mlima Kenya.

Rigathi Gachagua alitangaza kwamba wale ambao watapatikana wakiuza pombe haramu watakamatwa na kuchuliwa hatua kali na serikali. Raila Odinga kwa upande wake amemkashifu kwa kumwambia akome kuwakamata vijana wanaokunywa pombe kwa sababu hawana kingine wanachoweza kufanya.

Raila Odinga alimweleza Rigathi Gachagua kuwa ikiwa anataka vijana wakome unywaji pombe basi awape kazi.

Raila Odinga aliongeza kuwa bila ajira kwa vijana, basi kunywa pombe ndiyo njia ya kwenda. Uchumi ni mgumu sana kwa watu wasio na kazi kustahimili.

HUku aliyekuwa mgombea mwenza wake Martha Karua akizungumza wakati wa mkutano siku ya Alhamisi alisema kuwa maisha yamekuwa magumu sana kwa watu kustahimili.

"Ata wale wake Sugoi wanalia njaa, bei ya unga bado haijashuka, watakuja kuwadanganya muende mrengo yao hati hutasumbuka, lakini niko hapa kuwaambia kila mtu anaumia kiuchumi,                      

2022, kura zetu zillibwa peupe pale Bomas. Hatutakubali kura zizidi kuibwa kila uchao. Ili tumalize tatizo hili, ni sharti server zifunguliwe ibainike ushindi ulikuwa wa nani."