Ibada ya Kilifi: Mili 6 zaidi yafukuliwa katika shamba la mchungaji MacKenzie

Mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie angali anazuiliwa na polisi.

Muhtasari

• Idadi ya miili iliyofukuliwa sasa imefikia  27 .

•Siku ya Jumamosi, miili 14 ilipatikana, ikiwemo miili mitano, inayoaminika kuwa ya familia moja

waanza kuopoa miili ya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kasisi wa Malindi Paul Mackenzie katika eneo bunge la Shakahola Magarini kaunti ya Kilifi.
Maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha mauaji na wataalam wa uchunguzi waanza kuopoa miili ya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa kasisi wa Malindi Paul Mackenzie katika eneo bunge la Shakahola Magarini kaunti ya Kilifi.
Image: ALPHONSE GARI

Maafisa wa upelelezi wa mauaji siku ya Jumapili walifukua miili sita zaidi ya waathiriwa katika dhehebu la kanisa la Kilifi.

Hii inafikisha idadi ya miili iliyofukuliwa kuwa 27.

Mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie angali anazuiliwa na polisi.

Siku ya Jumamosi, miili 14 ilipatikana, ikiwemo miili mitano, inayoaminika kuwa ya familia moja. Walizikwa pamoja.

Katika kaburi jingine, miili mitatu ilipatikana juu ya kila mmoja.

"Tulimpata, mwanamume, mwanamke na watoto watatu kwenye kaburi moja," mpelelezi alisema

Miongoni mwa miili iliyofukuliwa, watoto walikuwa wengi ikilinganishwa na watu wazima.

Kufikia Ijumaa makaburi 58 yalikuwa yametambuliwa.

Mhubiri huyo matata wa Malindi amekuwa akiwahubiria wafuasi wake kufunga na kuomba kwa siku kadhaa na hatimaye, baadhi yao kufariki kutokana na njaa.

Mwezi uliopita, Mackenzie alikamatwa na maafisa wa polisi kutokana na kifo cha watoto wawili katika hali sawa lakini akaachiliwa kwa bondi ya polisi ya Sh10,000.

Inadaiwa kuwa waathiriwa walikuwa wamevurugwa akili, kwa mujibu wa polisi.