Habari za hivi sasa - Mjane wa Dedan Kimathi, Mukami Kimathi afariki, 96

Kulingana na bintiye Everlyn Kimathi Wangui, mama Mukami alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa .

Muhtasari

• Alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kupata matatizo ya kupumua.

Mjane wa shujaa wa Mau Mau Dedan Kimathi, Mukami Kimathi.
Mjane wa shujaa wa Mau Mau Dedan Kimathi, Mukami Kimathi.
Image: HISANI

Mjane wa shujaa wa kupigania uhuru wa taifa la Kenya, Field Marshal Dedan Kimathi, Mukami Kimathi amefariki.

Mama Mukami ambaye pia ni shujaa wa ukombozi wa Kenya kutoka minyororo ya ukoloni amefariki akiwa na umri wa miaka 96.

Alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kupata matatizo ya kupumua.

Kulingana na bintiye Everlyn Kimathi Wangui, mama Mukami alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa .

Mukami atakumbukwa sana kwa mchango wake wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Kenya. Alikuwa miongoni mwa wanawake shujaa waliokuwa wakiwapelekea chakula wapiganaji wa Mau Mau wakiwa msituni.