Canada yakanusha kutoa fursa ya ajira kwa Wakenya

IRCC ilisema kwa taarifa sahihi kuhusu jinsi ya kuhamia Canada, Wakenya wanapaswa kutembelea tovuti ya uhamiaji nchini humo.

Muhtasari
  • Haya yanajiri kufuatia tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua Jumanne kwamba Wakenya sasa wataweza kwenda kuishi au kufanya kazi nchini Canada.

Serikali ya Canada imekanusha ripoti kuwa Wakenya sasa wanaweza kusafiri hadi nchini humo kutafuta nafasi za kazi.

Haya yanajiri kufuatia tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua Jumanne kwamba Wakenya sasa wataweza kwenda kuishi au kufanya kazi nchini Canada.

Waziri Mutua, ambaye alikuwa katika ziara rasmi nchini, alisema alifanya mkutano na Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa Canada (IRCC) Sean Fraser na kukubaliana kuhusu fursa mbalimbali za uhamiaji.

Alisema mchakato kwa wanaotaka kwenda Canada ni rahisi lakini unahitaji bidii. "Taarifa potofu zinasambaa ambazo zinapendekeza kuwa programu maalum zinakaribisha wahamiaji wa Kenya.

Huu ni uongo, na programu za uhamiaji zilizotajwa hazipo," IRCC ilisema katika taarifa.

IRCC ilisema kwa taarifa sahihi kuhusu jinsi ya kuhamia Canada, Wakenya wanapaswa kutembelea tovuti ya uhamiaji nchini humo.