Maseneta Sifuna na Khalwale kuongoza mazungumzo kuhusu IEBC

Kamati ndogo yenye wanachama sita itajadili mageuzi katika tume ya IEBC.

Muhtasari

• Ujumbe wa Kenya Kwanza utajumuisha Seneta wa Bomet Hillary Sigei, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse.

b6251efb2cdb00bc
b6251efb2cdb00bc

Kamati ya pande mbili inayoshirikisha miungano ya Kenya kwanza na Azimio imeunda kamati ndogo ya wanachama sita kujadili mageuzi katika tume ya IEBC.

Akihutubia wanahabari, mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo ya pande mbili Otiende Amollo alisema Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ataongoza upande wa Azimio, huku Seneta wa Kakamega Boni Khalwale akiongoza upande wa Kenya Kwanza.

Wawakilishi wa Azimio ni kama ifuatavyo: Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Seneta wa Kitui Enoch Wambua na Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo.

Ujumbe wa Kenya Kwanza utajumuisha Seneta wa Bomet Hillary Sigei, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse.